Car Features

Mfumo wa Breki wa Gari: Uchambuzi wa Kina (Brake System)

https://www.yourmechanic.com/
#SpaceYaMagari

Huu ni mfumo katika gari unaomuwezesha dereva kupunguza mwendo wa gari na kusimama, brake za gari husika zimetengenezwa kukizi mahitaji ya gari husika, mfano kadiri gari linavyoongezeka uzito pia brake force inatakiwa pia iongezeke. Nguvu ya mguu wa binadamu haiwezi kusimamisha gari kiuhalisia hivyo tunahitaji nguvu ya ziada itakayo msaidia dereva kutumia brake.

https://www.howacarworks.com/

Mechanical brakes system.

Hizi ni brake ambazo nguvu ya binadam ndiyo hutumika kusimamisha gari, brake hizi mara nyingi hutumika kwenye pikipiki na baiskel. Pia hutumika kama parking brake kwenye magari.

Hydraulic brake system.

Huu ni mfumo wa brake ambao nguvu ya binadam (mechanical energy) inabadilishwa kua hydraulic energy inayoenda kushika brake kwenye matairi,. Kuna kua na master cylinder ambapo hydraulic inasukumwa na piston ili kutengeneza presha, presha ikitengenezwa inaenda kusukuma piston zilizoko kwenye wheel cylinder ili brake zishikwe. Mfumo huu wa brake hutumika kwenye magari madogo pamoja na pikipiki.

www.theengineerspost.com

Hydo-pneumatic brake system.

Huu ni mfumo unaotumia vyote hydraulic pamoja na upepo. Dereva akikanyaga brake anaruhusu upepo utoke kwenye reservoir tank kwenda kusukuma piston iliopo kwenye master cylinder ili hydraulic isukumwe kwenda kwenye wheel cylinder. Mfumo huu hupatikana kwenye magari ya kati (medium duty vehicles) mfano fuso fighter, isuzu  forward, etc.

Pneumatic or air brake system.

Huu ni mfumo unatumia upepo kusukuma brake. Dereva anapokanyaga brake anaruhusu upepo uende kwenye air chamber(wabongo wanaita booster) kusukuma diaphragm ili isukume push rod, push rod inazungusha s-cam, s-cam inatanua brake shoe na brake zinapatikana. Hizi ndo brake zenye nguvu na salama kuliko zote, upepo unapoisha kwenye system spring brake automatically inasukuma push rod ili gari isimame, kwenye huu mfumo spring brake inatumika kama parking brake (wabongo wanaita hendibreki) ndo mana gari kubwa iki park lazima dereva amwage upepo kwenye system.

Kumbuka upepo ukishatumika haufai kurudisha kwenye tank ni lazima uumwage nje. Kwa wale wanaoendesha hydo-pneumatic brakes kuwen makini hua upepo ukiisha huwezi kupata brake.

https://enginemechanics.tpub.com/

Aina za brakes.

Brakes ziko za aina nyingi sana ila zinazotumika kwenye magar ni mbili tu.

Drum brakes.

Hizi ni brake ambazo zinakua na shoe. Brake inapokanyagwa either kwa nguvu ya mechanical, hydraulic au upepo brake shoe zinatanuka kushika drum na drum imefungiwa na tairi kwaiyo gari litapunguza mwendo au kusimama kabisa

https://www.howacarworks.com/

Faida za drum brake.

  • -Zinatumuka kwenye magari yote, makubwa na madogo na hata pikipiki
  • -Drum ni nzito, kutokana na uzito huu ni ngum kupata moto hadi brake zisishike.
  • -Kuna uwezekano wa kutumika vyovyote eitha mechanical, hydraulic au upepo.

Hasara za drum brake.

  • Zinahitaji udjustment za mara kwa mara
  • Wheel cylinder ikivuja hupati brake
  • Zinachukua mda mref kufanyia service.

Disc brakes.

Hizi ni brake zinakuaga na brake pads zinazoshikilia disc au rotor. Brake zinapokanyagwa nguvu ya hydraulic au upepo inaminya brake pads ili zishikilie rotor isizunguke ili tupate brake

https://www.yourmechanic.com/

Faida za disc brake.

-zina brake force kubwa kuliko drum brake
-Hazina haja ya kuadjast mara kwa mara
-Hata wheel cylinder ikivuja brake zinapatikana
-Stopping distance ni ndogo ukilinganisha na drum brake.

Hasara za disc brakes.

-kutokana na udogo wake zinapata moto, na zikipata moto friction force inapungua hivyo basi brake hazikamati.
-Hazifai kutumiwa mechanically, hivyo basi hazina parking brake.

https://www.motortrend.com/

Mwisho, magari mengi nyuma yanatumia drum brakes na mbele ni disc brakes ila pia kuna yanatumia drum brake kote mbele na nyuma pia kuna yanayotumia disc mbele na nyuma kote lakini nyuma zinakua zote mbili ili tupate parking brake

Unaponunua gari soma user manual ili kujua specifications za gari husika. Ushauri, ukinunua gari kabla hujaweka mafuta ya brake angalia juu ya mfuniko kujua ni mafuta ya aina gani yanatumika katika gari husika mara nyingi kuna DOT 3 na DOT 4

+ posts
#SpaceYaMagari

1 Comment

Leave a Reply