Car Reviews

IJUE 𝗩𝗼𝗹𝗸𝘀𝘄𝗮𝗴𝗲𝗻 𝗚𝗼𝗹𝗳

#SpaceYaMagari

Gari hii imekua mojawapo ya gari inayokubalika sana Duniani.

Up to December, 2021. Zaidi ya Volkswagen Golf 35,000,000 ziliuzwa.

Model hii ndio Best Seller wa VW! Fasten your seat belt!, Ladies and Gentlemen, hebu tuijadili model hii…

Volkswagen ni neno la Kijerumani linalomaanisha “𝑇ℎ𝑒 𝑝𝑒𝑜𝑝𝑙𝑒’𝑠 𝐶𝑎𝑟” Wajerumani walianza kuzalisha gari hii aina ya Golf mnamo mwaka 1974. Gari hii ambayo ni 𝐶𝑜𝑚𝑝𝑎𝑐𝑡 𝐹𝑎𝑚𝑖𝑙𝑦 𝐶𝑎𝑟 imekubalika dunia nzima ndio maana mpaka sasa wanaendelea kuzizalisha.

Volkswagen Golf ina Generation 8. Generation ya kwanza ilitoka mwaka 1974 na ikawa mbadala wa previous model ambayo ni 𝑉𝑜𝑙𝑘𝑠𝑤𝑎𝑔𝑒𝑛 𝐵𝑒𝑒𝑡𝑙𝑒. Generation hii inajulikana kama MK1 Ilibeba engine ndogo hivyo matumizi yake ya mafuta yalikua ni very economical…👇🏽

Mk1 ilipewa nguvu na 1,093 CC inline four-cylinder {single over head cam} SOHC engine. Engine hii ni ndogo zaidi kwenye generation za Volkswagen Golf. Gari hii ilikua hatchback ya milango 3 na nyingine zilikua milango 5.

Courtesy

Mnamo mwaka 1976 kampuni ya Volkswagen walitoa model aina ya GTI. Model hii ilikuja na engine ambayo ni 1.6L na iliweza kufika 180km/h. Mwaka huu pia walifanikiwa kutoa Volkswagen golf inayotumia Diesel. Generation hii ikaisha kibabe, sasa VW ana Petrol na Diesel Engine…

Generation ya pili ilitoka mwaka 1983 na iliitwa MK2. Japokua mwonekano wake ni kama MK1, ila hii ilikua ndefu kiasi. MK2 ilibuniwa na mtaalam Herbert Schäfer. Gari hii iliingia sokoni na transmission kama vile: 4-speed manual, 5-speed manual Na 3-speed AT.

Courtesy

Upande wa engine, MK2 aliingia na, EA111 l4 (1.0L, 1.3L) na 1.6L EA827 l4 petrol engines. Huku upande wa diesel engine alibeba 1.6L EA827 l4. Wakatoa na Turbo diesel pia ila engine haikubadilishwa. Generation hii pia ndio ilikua mwisho wa Carburettor petrol engine.

Third Generation ya Volkswagen Golf ilitoka mnamo mwaka 1991. Generation hii iliwapa Volkswagen fahari kubwa maana ilishinda tuzo za kutosha!. Hapa walitoa gari hii ikiwa na Turbocharged Direct Injection (TDI) 2.8L VR6 engine.

Courtesy

Kwenye matumizi ya mafuta hapa walikua sawa maana inaenda 9L/100Km Chini ya generation hii Volkswagen walitoa models kama vile Golf Estate , Cabriolet, na Vento miaka ya 1993, 1995 na 1999 respectively.

Fourth Generation ya Golf ilianza mwaka 1997 – 2006. Hapa Volkswagen walichofanya wao ni kuingia sokoni na norback version. Pia walifanya facelift kwa models nyingi za 3rd Generation. Mabadiliko makubwa yalikua kwenye engine bana…

Walitengeneza a World class engine ambayo ilikua na 3.2L VR6 ambayo iliwekwa kwenye 4-wheel drive ya model mpya ya Golf R32 mnamo mwaka 2002. Engine ndogo yake ilikua ni 2.0L 8-valve SOHC. Four cylinder gasoline engine ambayo iliwekwa 6-speed AT.

Courtesy

Generation ya 5 Ilitoka mwaka 2003 Generation hii ilikuja na 2.5L, 5-cylinder engine inayoweza kuzalisha 150Hp na miaka ya mbele engine hio iliongezewa HP’s mpaka kufika 170. Pia hapa walitoa GTI version ambayo ilizalisha 197HP kutoka turbo engine ya FSI.

Generation ya 6 (MK6) ya Volkswagen Golf ilibuniwa na Walter de’Silva mwaka 2008. Hapa bana walitoa gari ambayo iliondoa sifa mbaya zote, walitoa gari ambayo ni fuel efficient na halina kelele yoyote. Hii ni Luxurious Golf! Generation hii ilikuja na 3 engines ambazo ni…

2.0L 4-cylinder clean diesel. Ambayo ilizalisha 134HP. 2.5L inline 5-cylinder petrol engine. Ambayo ilizalisha 174HP GTI Version ilikuja na Turbocharged TFSI inline 4 engine. Engine hizi zilikua na AT na MT zenye 6 speed.

Generation ya 7 (MK7) ilitoka rasmi mwaka 2012 kwenye maonyesho makubwa zaidi duniani yanayojulikana kama Paris Motor Show. MK7 lilikua kubwa kiasi kuliko MK6 lakini jambo la ajabu ni kwamba lilikua na uzito mdogo kuliko MK6. Hapa waliitangaza model mpya iitwayo…

Volkswagen Golf R. Model hii ilikua na maboresho makubwa hasa upande wa mwonekano na nguvu za engine. Engine za R zilikua ni, 1.5L TSI EVO ambayo ilizalisha 130HP. Waliweka pia LED lights, na animated tail indicator (hii ipo kwenye Audi pia)

Kwa wale wapenzi wa Powerful cars. Golf R walitoa 2.0L Turbocharged EA888 petrol FSI inline 4 engine. Inayozalisha 296bhp. Engine hii inapatikana kwenye Golf GTI na Audi S3.

Currently Volkswagen Golf ipo kwenye Generation ya 8.

Mnamo mwaka 2019 Generation hii ilitangazwa jijini Wolfsburg Wakati wanaitoa hii gari waliweka model ya 5 door Hatchback kwakua ile ya milango 3 iliwapa shida kwenye mauzo. Generation hii ninaweza sema ndio Best kuliko…

Mwonekano wa ndani umepewa sura mpya kabisa na wameweka latest Tech kwenye mifumo yote. Features kama vile, Digital cockpit, Travel assist, adaptive cruise control, as well as lane-keeping control system

Usukani wake una sensor. Usipogusa usukani ndani ya sekunde 15 pekee, ABS ambayo ni automatic italazimika isimamishe gari. Dah VW let me salute you!!

Upande wa engine pia wameleta Mapinduzi… Hapa kuna powertrain za aina tatu. 1/ Compact Petrol 2/ Diesel na 3/ Hybrid. Engine imetumika ileile ya 7th Generation, ambayo ni VW EA888 2.0L Turbocharged 4-cylinder unit.

Gari hii ipo na nguvu na speed nzuri sana, inaenda 0-100kmh ndani ya sekunde 7 pekee. Gari hii inakua na mfumo iitwayo Vehicle Dynamics Manager ambayo inaongoza differential (difu) na new adaptive dampers, Mara 200 kila sekunde.

Courtesy

+ posts
#SpaceYaMagari

Leave a Reply